Kibodi ya Google Automotive ina mambo yote unayopenda kuhusu Kibodi ya Google: Kasi, Kutegemewa, Kuandika kwa Kutelezesha Kidole, Kuandika kwa Kutamka, Kuandika kwa mikono na zaidi
Kuandika kwa kutamka — Tamka maandishi kwa urahisi popote ulipo
Kuandika kwa Kutelezesha Kidole — Andika haraka zaidi kwa kutelezesha kidole chako kutoka herufi hadi herufi
Kuandika kwa mikono — Andika kwa ufasaha na herufi zilizochapishwa
Lugha zinazotumika ni pamoja na:
Kiarabu, Kichina, Kicheki, Kiholanzi, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kigiriki, Kiindonesia, Kiitaliano, Kijapani, Kinorwe, Kipolandi, Kireno, Kiromania, Kirusi, Kihispania, Kiswidi, Kithai, Kituruki, Kiyukrania na nyingine nyingi!
Vidokezo vya kina:
• Kusogeza kiteuzi: Telezesha kidole chako katika upau wa nafasi ili usogeze kiteuzi
• Kuweka lugha:
1. Nenda kwenye Mipangilio → Mfumo → Lugha na uwekaji data → Kibodi → Kibodi ya Google Automotive
2. Chagua lugha unayotaka kuweka. Aikoni ya dunia itaonekana kwenye kibodi
• Kubadilisha lugha: Gusa aikoni ya dunia ili ubadilishe kati ya lugha zinazotumika
• Kuangalia lugha zote Bonyeza kwa muda mrefu aikoni ya dunia ili uone orodha ya lugha zote zinazotumika kwenye kibodi
Ilisasishwa tarehe
7 Apr 2025